SIMBA YATOA TAMKO KUHUSIANA NA MASHABIKI WAKE, TAIFA STARS VS UGANDA


Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake, Haji Manara, umesema sakata la wachezaji wake na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeshamalizika hivyo amewaomba watanzania wote waisapoti timu hiyo.

Kauli ya Manara imekuja kufuatia Kocha Mkuu wa Stars, Emmanuel Amunike kuwaondoa wachezaji 6 wa Simba baada ya kuchelewa kuripoti kambini, lakini baadaye alikutana na kuzungumza nao kisha kuwasamehe.

Kutokana na kitendo cha Amunike kuwasamehe wachezaji hao, Manara amewaomba watanzania wote wakaipe sapoti timu ya taifa itakapocheza na Uganda hasusani waliopo kanda ya ziwa.

Ofisa huyo amesema hakuna haja ya kuitenga timu kutokana na na baadhi ya mashabiki wa Simba kuibuka na kueleza wataisaliti kwa kuipa sapoti Uganda baada ya kupatwa na hasira sababu za wachezaji wao kuondolewa.

Stars itacheza na Uganda Septemba 8 huko Kampala ukiwa ni mchezo wa kufuzu kuelekea fainali za AFCON 2019.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post