Gari ya Peter Msechu Balaa!!! “Kila Nikitafuna inajizima”



Staa kutokea kwenye muziki wa Bongo FlevaPeter Msechu ametoa kali ya mwaka Gari ya Peter Msechu balaa!!! “kila nikitafuna inajizima”  kuwaacha mashabiki wake midomo wazi baada ya kumnunulia mke wake gari aina ya Toyota Porte mwaka 2015.

Peter Msechu ametumia ukurasa wake wa instagram na kusema kuwa alimnunulia mke wake gari hilo kutokana na marafiki wa mke wake kumnyali kwa kukosa gari, hivyo akaona sio vibaya kumnunulia usafiri na yeye pia.

Peter Msechu ameandika “Gari langu la tatu mwaka 2015 nilimnunulia Mama Lolo gari hii baada ya kuona mashost zake wanamnyali sana, ila sijui Mama Lolo aligongesha wapi maana lilianza  kuwa bovu balaa ugonjwa wake kila hospitali walishindwa”

“Kuna muda lilikuwa linawasha wiper tu bila sababu mara unashangaa honi inajipiga tu yenyewe bila kubonyezwa Kuna siku ndio nilichoka kabisa ilikuwa haina mafuta kabisa taa imewaka na nikawa sina hela ya mafuta ila nikapita mahali kuchukua chips nilie kwenye gari”

“Kumbe akamaind kila nikitafuna inajizima nisipotafuna inawaka hii ndio gari pekee ambayo imetoka Japan haikuwahi kuzima taa ya mafuta”

‘Taa ya mafuta ilikuwa inawaka mpaka dashboard inakua ya moto  vitu kama mayai ya mjusi kuyakuta katikati ya siti za kukalia ilikuwa kawaida tu #KISIRANI story ya gari la nne na la tano zitakujia mnamo kesho jioni kuanzia saa 1 jioni ita wenzako wakae tayari”


Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post