RASMI: NGASSA AANZA MAZOEZI NA YANGA


Mrisho Ngassa amerejea Yanga rasmi baada ya kuanza mazoezi leo.

Ngassa ameanza mazoezi na kikosi cha Yanga kwenye Uwanja wa Polisi jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kuanza mazoezi, Ngassa bado hajamalizana na Yanga lakini yuko katika hatua nzuri.

Mwenyewe amekuwa hataki kulizungumzia suala hilo lakini rafiki yake wa karibu amesema wanakaribia kumalizana.

“Imebaki kidogo tu watamalizana na Yanga, ameona aanze mazoezi kwa kuwa wako ukingoni,” alisema.

Ngassa anarejea Yanga kwa mara ya tatu, safari hii akitokea Ndanda FC ambayo ilinusurika kuteremka daraja msimu uliopita.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post