YANGA WATAJA SABABU YA KUJIONDOA KWENYE MICHUANO YA KAGAME CUP



Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amethibitisha kuwa ni kweli klabu hiyo imeandika barua kwa TFF kuitaarifu kuwa haitashiriki mashindano ya CECAFA Kagame Cup yanayotarajiwa kuanza Juni 28, 2018.

Ten amesema Kamati ya Mashindano ya Yanga imefikia uamuzi huo ili kulinda maslahi ya timu hiyo inayoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Msemaji huyo wa Yanga amesema wachezaji wa Yanga wamekuwa wakishiriki mashindano mengi msimu huu bila ya kupumzika.

"Hivi sasa wachezaji wamepewa likizo na wanatarajiwa kurudi kambini Juni 25, 2018 kuanza maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia,"amesema Ten.

Ten ameongeza kuwa ratiba ya michuano ya kombe la Kagame inaonyesha mchezo wa fainali utapigwa Julai 13 wakati Yanga inatarajiwa kucheza na Gor Mahia kati ya Julai 16-18.

Hivyo wameona ni vyema wachezaji wakaachwa wapate mapumziko ya kutosha kabla ya kurejea kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Gor Mahia na msimu mpya.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post