UAMUZI WA ZIDANE WAISHANGAZA DUNIA


Zinedine Zidane anaachia ngazi Real Madrid: Je Real Madrid itafanya nini?

Zidane alitangaza uamuzi wake katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo uwanja wa Valdebebas

''Uamuzi wake ulikuwa kama mlipuko wa bomu''

Aliondoka kama vile alivyowasili na alivyohudumia miaka yake miwili na nusu akipewa heshima kubwa. Uamuzi wa Zidane kuondoa katika klabu ya Real Madrid siku tano baada ya kuiongoza klabu hiyo kushinda kombe lake la tatu la vilabu bingwa mfululizo umewaacha mabingwa hao wa Uhispania na kizaa-zaa.

Rais wa klabu hiyo Florentino Perez alishangazwa na uamuzi huo , ambao Zidane aliutoa katika mkutano na vyombo vya habari siiku ya Alhamisi na sasa maafisa wa ngazi za juu katika uwanja huo watalazimika kufanya kazi ya ziada kumtafuta na kumfichua kocha atakayemrithi raia huyo wa Ufaransa.

Vyombo vya habari vya Uhispania pia vilipigwa na butwaa.

Habari kutoka katika mtandao wa Marca zilisema alikishangaza chumba cha maandalizi kama ''mlipuko wa bomu'', huku gazeti la El Mundo likisema katika kichwa chake cha habari ''Real Madrid haijaamini kwamba kunaweza kuwa na nahodha bora katika jahazi hilo gumu''.

Hatahivyo BBC inaangazia sababu za Zidane kuondoka na maana yake kwa mabingwa hao wa Ulaya.

Je uamuzi wake wa kujiuzulu umewashangaza wengi?

Zinedine Zidane amekuwa kocha wa kwanza duniani kushinda kombe la vilabu bingwa mara tatu mfululizo

Ni kweli kwamba habari za kujiuzulu kwake zilimshangaza rais wa klabu hiyo Florentino Perez ambaye alitumia wakati mwingi wa mkutano huo na vyombo vya habari akionekana kama mtu aliyekosa jawabu katika uso wake akijaribu kuamini kile alichokuwa akisikia.

Perez alitangaza kwamba Zidane alimwambia kuhusu uamuzi wake siku iliopita, huku naye {Zidane} akifichua kwamba mchezaji wa pekee aliyezungumza naye kuhusu uamuzi wake ni nahodha Sergio Ramos.

Zidane alikuwa wazi kuhusu sababu zake za kuondoka , akikiri kwamba hajui atakavyoisaidia timu hiyo kuibuka mshindi msimu ujao huku akisisitiza kuwa timu hiyo inahitaji damu mpya mbali na kuzungumzia kuhusu shinikizo kali na mahitaji katika wadhfa huo.

Hakusema ni lini aliamua kuchukua uamuzi huo, lakini kulikuwa na ishara kadhaa, wakati alipoulizwa kutaja wakati wake mgumu wakati wa kipndi chake cha ukufunzi , Zidane hakusita kusema kuwa kombe la Copa del Rey ambapo timu hiyo ilibanduliwa na Leganes mnamo mwezi Januari.

Na swali la mwisho lililomkabili kabla ya kuondoka katika mkutano huo na klabu hiyo huku akishangiliwa ni iwapo alidhani kwamba ulikuwa wakati mwafaka kuondoka katika klabu hiyo baada ya kushinda taji lake la tatu la vilabu bingwa.

Zidane alitabasamu na kujibu ''pengine , pengine ni kweli''.

Je Real inapanga kufanya uamuzi gani?

Rekodi ya Zidane akiwa Real MadridMashindano:GWDLGFGAW%Ligi ya Uhispania9668181026310170.8Vilabu bingwa332274783766.7Copa Del Rey12642331550Fifa Club World Cup440093100Uefa Super Cup220053100Supercopa Uhispania220051100Jumla149104291639316069.8

Baadhi ya majina yanasambazwa kuonyesha ni nani atakayemrithi Zidane, huku mkufunzi anayepigiwa upatu kumrithi akiwa Mauricio Pochettino.

Inaaminika mkufunzi huyo wa Tottenham huenda akawa chaguo la kwanza la Perez: Amempenda Pochettino tangu alipokuwa katika ligi ya La Liga akiifunza Espanyol, klabu ambayo Real ina uhusiano wa kirafiki na alifurahishwa na matokeo ya klabu hiyo ya Uingereza wakati iliposhiriki katika kombe la vilabu bingwa msimu huu.

Maurico Pochettino

Kizuizi ni kwamba Pochetino alitia saini kandarasi ya miaka mitano katika klabu ya Spurs , raia huo wa Argentina huenda akakataa kujiunga na klabu hiyo muda mfupi baada ya kutia saini kandarasi mpya hata ijapokuwa kuna uvumi kwamba kandarasi hiyo mpya ina kipengee kinachoweza kumruhusu kuondoka iwapo Real Madrid inamuhitaji.

Antonio Conte

Mkufunzi mwengine anayepigiwa upatu ni kocha wa Chelsea Antonio Conte-ijapokuwa raia huyo wa Italy anaweza kuwa mtu asiyeweza kudhibitiwa na Perez, anayependelea wakufunzi ambao anaweza kuwadhibiti mbali na kuwa na falsafa ya mashambulizi.

Joachim Low

Mkufunzi wa timu ya taifa la Ujerumani Joachim Low pia anahusishwa na kazi hiyo , lakini hakuna matumani makubwa baada ya hivi karibuni kutia saini kandarasi ya miaka minne huku akionekana kutokuwa na tatizo lolote kusalia katika klabu hiyo, huku Perez pia akitarajiwa kuvamia klabu ya Napoli na kumnyakua kocha wake Maurizo Sarri anayedaiwa kujiandaa kujiunga na Chelsea ama hata Jose Mourinho kutoka Manchester United.

Na pengine kuna mkufunzi mwengi anayeheshimika na kupendwa ambaye huenda akaangaziwa. ''Aondoka Zizou aingia Arsene Wenger''?

Bale na Ronaldo kuondoka, Neymar kujiunga na Real Madrid?

Wakati pekee ambao Zidane alionekana kukasirishwa wakati wa mkutano wake wa mwisho na vyombo vya habari ni pale alipoulizwa iwapo hatma ya Cristiano Ronaldo katika klabu hiyo ndio iliomshinikiza kufanya uamuzi huo .

Alijibu mara moja na kusema hapana, hapana kabisa.

Ronaldo na Gareth Bale

Hatahivyo yule atakayemrithi Zidane atakuwa na maswala tata kukabiliana nayo kuhusu hatma za Ronaldo na Gareth Bale.

Swala la Neymar kujiunga na Madrid huku kukiwa na ripoti katika vyombo vya habari vya Uhispania vikisisitiza kwamba nyota huyo wa PSG yuko tayari kutafuta njia ya kuondoka PSG msimu huu.

Pengine swali nyeti ni kwa kiwango kipi mkufunzi huyo mpya atakuwa na usemi katika swala hilo, wakati wa kuajiriwa kwa mkufunzi mpya mbali na pendekezo la Perez kuwa na ushawishi kuhusu maswala ya kibinifasi kunamaanisha kwamba mkufunzi mpya atepewa kikosi badala ya kuwachwa kukichagua.

Neymar

Kutakuwa na mengi ya kutazama ikiwemo uwezekano wa Kipa Keylor Navas kupigwa teke na nafasi yake kuchukuliwa na Thibaut Courtois ama David de Gea.

Je Luka Modric anatimiza umri wa miaka 33, je nafasi yake inafaa kuchukuliwa?, je ni wakati wa Karim Bnezema kuondoka, je nyota kinda Marco Asensio anafaa kukuzwa ? Je Eden Hazard, Robert Lewandowski au Mohamed Salah wanalengwa katika dirisha la uhamisho?

Luca Modric

Kitu muhimu , ni kwamba kundi lolote la wachezaji ambalo atapatiwa mkufunzi mpya , ataamua na kutekeleza mbinu mpya ya mchezo kitu ambacho hakikuonekana chini ya usimamizi wa Zizou swala linalotilia mkazo thibitisho kwamba hajui iwapo angeweza kuendeleza ufanisi wa klabu hiyo.

Je Zidane anaelekea wapi?

Hatahivyo yule atakayemrithi Zidane atakuwa na maswala tata kukabiliana nayo kuhusu hatma za Ronaldo na Gareth Bale.

Ajabu- ni kwamba licha ya kushinda mataji matatu ya vilabu bingwa mfululizo na kuongeza jumla ya mataji kuwa tisa katika misimu miwili, kuna swali kubwa kuhusu uwezo wa Zidane kufunza soka.

Raia huyo wa Ufaransa ametajwa kuwa na bahati na wapinzani wake-hususan kutokana na mwelekeo wa Barcelona , na ijapokuwa hiyo sio sababu ya kutosha ya mafanikio yake sio ukweli kwamba uwezo wake wa kiufundi unatiliwa shaka.

Alirithi timu yenye wachezaji nyota , na hakuna hata mchezaji mmoja wa 2017 au 2018 aliyesajiliwa na zidane.

Didier Deschamps

Uwezo mkubwa katika klabu hiyo ilikuwa kudhibiti tabia za nyota hao katika chumba cha maandalizi na hivyobasi kupata heshima kubwa kutoka kwa wachezaji wake na kumfanya kila mtu kuwa na maono sawa katika mazingira ambayo yamekumbwa na utata katika siku za nyuma.

Licha ya kwamba angenyatiwa na vilabu vikubwa msimu ujao , Zidane kwa sasa anasema kwamba hana haja , hatafuti klabu mpya na kwamba hana mpango wa kuwa mkufunzi msimu ujao.

Arsene Wenger

Kulingana na ubora wake anaweza kuwa kocha mzuri wa kimataifa. Iwapo Didier Deschamps atashindwa kupata matokeo mazuri kutoka kwa kikosi chenye wachezaji wenye vipawa wakati wa kombe la dunia , atapigiwa upatu kumrithi.

Tukiangazia uhusiano mzuri aliokuwa nao na rais wa Real Madrid Perez, musishangae iwapo Zidane atarudi tena Bernabeu katika siku za usoni . Kama alivyoanza katika mkutano wake na vyombo vya habari ''tuonane tena baadaye'' badala ya ''kwaheri''.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post