TIMU NYINGINE YAJIONDOA KWENYE MASHINDANO YA KAGAME CUP


Mabingwa wa Ethiopia St George wameungana na Yanga kujiondoa kwenye michuano ya kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza wiki ijayo Juni 29 jijini Dar es salaam.

Timu zote zilikuwa kundi C hivyo kufanya kundi hilo kubaki na timu mbili pekee Simba na Dakadaha ya Somalia

Kulingana na ratiba mpya iliyotolewa, nafasi za Yanga na St George katika kundi C zimechukuliwa na vilabu vya Singida United na APR ya Rwanda huku Vipers FC ikipelekwa kundi A.

Michuano hiyo itachezwa katika viwanja vya Azam Complex Chamazi na uwanja wa Taifa.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post