TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATANO 20.06.2018

 Wilfried Zaha


Huddersfield wanatarajia kuwashinda Southampton na Lyon katika kumsaini mshambuliaji wa Ubelgiji kiungo wa kati Anthony Limbombe, 23, kutoka Brugge. (Sun)

West Brom wamekataa ofa ya kwanza ya Burley kwa mchezaji Jay Rodriguez, huku mshambuji huyo mwenye mika 28 akitarajiwa kurudi kwenye klabu yake ya zamani. (Mail)

 Maurizio Sarri

Ajenti wa Maurizio Sarri amewasili London na meneja huyo wa zamani wa Napoli mwenye miaka 59 ambaye anatarajiwa kuchukua mahala pake Antonio Conte kama meneja wa Chelsea. (Sky Sports)

Crystal Palace watampa ofa Wilfried Zaha ya puni milioni 120,000 kwa wiki kumzuia raia huyo wa Ivory Coast mweye miaka 25 ambaye ameivutia Tottenham. (Mirror)

 Moussa Konate
West Ham na Burnley wanashindana kumsaini mchezaji wa thamani ya pauni milioni 8 msenegal Moussa Konate, 25, kutoka klabu ya Ufaransa ya Ligue 1 Amiens. (Sun)
Southampton wanajiandaa kumwendea kiungo wa kati wa Red Bull Salzburg ambaye ni raia wa Mali Amadou Haidara, 20. (Mirror)

West Ham wanawinda mkataka wa thamani ya pauni milioni 35 kwa awing'a wa Lazio raia wa Brazil Felipe Anderson, 25. (Mail)

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post