Mohamed Salah Kustaafu Kuichezea Misri


Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri anayecheza club ya Liverpool ya England Mohamed Salah jina lake limezidi kuchukua headlines kiasi cha kudaiwa kutaka kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Misri.

Mohamed Salah anadaiwa kutaka kufanya hivyo baada ya picha yake  kiongozi wa kisisa wa Chechen Mr Ramzan Kadyrov kusambaa mitandaoni na kuanza kumkosoa staa huyo kwa kudai anatumika kisiasa, Ramzan ni kiongozi wa jimbo la Chechen nchini Urusi na amekuwa akidaiwa kuwa na sifa ambazo sio nzuri.

Hivyo kuonekana kwa MO Salah katika picha ya pamoja na kiongozi huyo kumezua maneno kiasi cha staa huyo kukasirishwa na kudaiwa kutaka kustaafu timu ya taifa kwani kuonekana katika picha ya pamoja na kiongozi huyo ni kama kumuunga mkono na matendo yake, MO Salah pia imeripotiwa kuwa amepewa uraia wa jimbo la Chechen.

Mashabiki wa soka nchini Misri baada ya kusikia taarifa za MO Salah kutaka kuachana na timu ya taifa kwa kuandamwa na maneno baada ya picha yake na Ramzan kusambaa, wameanza kupost ujumbe wenye #IamWithSalah kama njia ya kuonesha wapo pamoja nae na wasingependa astaafu, kama ufahamu timu ya taifa ya Misri imekuwa Chechen nchni Urusi kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post