Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa ameachia rasmi ngazi katika klabu yake baada ya mkataba wake kumalizika.
Nsajigwa aliingia katika benchi la ufundi la klabu hiyo wakati George Lwandamina akiwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho kabla ya ujio wa Mkongomani, Mwinyi Zahera.
Nsajigwa anaondoka Yanga ikiwa ni siku moja tu baada ya kuondolewa katika mashindano ya SportPesa Super Cup inayoendelea mjini Nakuru, huko Kenya.
Yanga iliondoshwa na Kakamega HomeBoys kwa mabao 3-1 Jumapili ya June 3 2018 uliopigwa kwenye Uwanja wa Afraha Stadium.
Kuondoka kwa Nsajigwa kutakuwa kunamfanya kocha Noel Mwandila kusalia kwenye benchi la ufundi la Yanga kama Msaidizi pekee