Huu ndio mpango wa Maradona kuinusuru Argentina World Cup 2018


Mkongwe wa soka duniani Diego Maradonaambaye aliisaidia timu yake ya Argentina katika fainali za Kombe la Dunia 1986, ametangaza kuomba nafasi ya kwenda katika mazoezi ya timu ya taifa ya Argentina kuelekea mchezo wake wake wa mwisho wa Kundi D dhidi ya Nigeria.

Argentina yupo katika hali mbaya na nafasi yake ya kufuzu hatua ya 16 bora matumaini yamerejea baada ya Nigeria kumfunga Icelandkwa magoli 2-0, hivyo Argentina ili afuzu hatua ya 16 bora, inabidi katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Nigeria apate ushindi huku akiombea Iceland ipate matokeo mabaya dhidi ya Croatia.

Maradona alinukuliwa na vyombo vya habari akieleza mpango wake anaoamini unaweza kuinusuru Argentina “Nataka kupata nafasi ya kwenda mazoezini na kuongea na wachezaji na kuwaeleza umuhimu wa kuvaa jezi ya timu ya taifa” 

Kwa sasa msimamo wa Kundi D lililopo na timu za Croatia, IcelandNigeria na Argentinalinaongozwa na Croatia waliofuzu tayari kwa kuwa na point 6, Nigeria nafasi ya pili kwa kuwa na point tatu, Iceland  nafasi ya tatu na Argentina wakiwa nafasi ya nne licha ya kufungana kwa point kuwa na point moja kila mmoja ila wametofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post