Fred anayetarajiwa kujiunga na Man United apata jeraha katika mazoezi


Fred alijeruhiwa wakati wa mazoezi ya timu ya Brazil mjini London UingerezaHaki miliki ya pichaPA
Image captionFred alijeruhiwa wakati wa mazoezi ya timu ya Brazil mjini London Uingereza
Kiungo wa kati wa Brazil Fred, anayetarajiwa kujiunga na klabu ya Manchester United amepata jeraha katika kifundo chake cha mguu katika mazoezi kabla ya kuanza kwa kombe la dunia.
United wamekubaliana dau la £47m kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutoka klabu ya Shakhtar Donetsk huku uhamisho huo ukitarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Maafisa wa soka akiwemo Mkenya wanaswa wakipokea fedha
Fred alipata jeraha kutokana na makabiliano na kiungo wa kati wa Brazil CasemiroHaki miliki ya pichaEPA
Image captionFred alipata jeraha kutokana na makabiliano na kiungo wa kati wa Brazil Casemiro
Daktari wa timu ya Brazil Rodrigo Lasmar alilitaja jeraha hilo lililotokea mjini London kuwa lenye maumivu makali katika mguu wake.
Brazil inaanza kampeni yake ya kombe la dunia dhidi ya Switzerland tarehe 17 mwezi Juni.
Alionekana kuwa na uchungu baada ya kifundo chake cha mguu wa kulia kufungwa bandejiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionAlionekana kuwa na uchungu baada ya kifundo chake cha mguu wa kulia kufungwa bandeji
Washindi hao mara tano wa kombe la dunia baadaye watacheza katika kundi E dhidi ya Costa Rica na Serbia nchini Urusi.
Lasmar aliongezea: kwa sasa ni mapema mno kusema chochote kuhusu hali yake. Siku ya Ijumaa tutaangalia tujue kitakachofanyikana kuamua iwapo tunahitaji kufanya uchunguzi wowote ama la.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post