Fahamu Chimbuko la POGBA


Pogba aliiwakilisha Ufaransa kila upande na alikuwa miongoni ma timu ya Euro 2016 iliopteza kwa Ureno katika fainali
Paul Pogba alianza kuvutia klabu kadhaa kabla ya ya kufikisha umri wa miaka 17 alipoondoka nyumbani na kujiunga na Manchester United kutoka klabu ya Ufaransa ya Le Havre.
Huku hatua hiyo ya kujiunga na Man United ikionekana kuwawacha wakufunzi wake na mshangao mkubwa, mchezaji huyo aliyekuwa na ari ya kutaka kufanikiwa hakushangaa.
Pogaba alijua kwamba alitaka kuwa mchezaji wa kulipwa tangu alipoanza kusakata soka katika vitongoji vya mji wa Paris pamoja na pacha wake-nduguye mkubwa.
Hizi ndio nambari zenye uzito katika Kombe la Dunia 2018
Lakini ni nini kinachomtofautisha mtu ambaye amewahi kushinda mataji ya nyumbani na Ulaya tofauti na wachezaji wenye ndoto kama yake ambao wamefeli kufanikiwa?
Baada ya kujiunga na Roissy -en-Brie akiwa na umri wa miaka sita hadi kutia saini kandarasi nchini Uingereza , muongo mmoja baadaye, BBC michezo inaangazia chimbuko la Pogba kupitia wale waliomjua sana.
'Paul alikuwa mtu ambaye alihitaji kuwa na mama mara kwa maraPaul Pogba alijiunga na Man United kwa daua lililovunja rekodi la £89m
Mtoto wa wazazi wa Guinea , Pogba alizaliwa mwezi machi 1993 na kulelewa katika jamii ya mashariki mwa Paris ya Lagny-sur-Marne pamoja na nduguye Florentin na Mathias.
Pacha hao , ambao ni wakubwa wake kwa miaka mitatu , pia walikuwa wachezaji wa kulipwa.
Licha ya wazazi wake kuachana , familia ya Pogba ilikuwa na jukumu kubwa katika ukuwaji wake wa soka , ikiwa na hamu kubwa na mchezo huo wakati alipojiunga na klabu yake ya kwanza Roissy-en-Brie, klabu hiyo ilikuwa maili chache kutoka nyumbani kwao.
Sambou Tati, rais wa klabu ya Roissy-en-Brie: "walilazimika kumpatia mahitaji yake yote kama vile wazazi wazuri wangemfanyia mwanao. Paul alikuwa kitinda mimba ambaye alihitaji mamake kila mara , hivyobasi mamake alimtelekeza kama vile alivyowafanyia pacha. Lakini huku Paul akiwa mdogo ,kweli, wakati unapokuwa kitinda mimba mara nyingi utashughulikiwa sana. Wazazi wake walimpenda sana.
'
Hakupenda kitu chengine chochote isipokuwa soka
Pogba alijiunga na Roissy akiwa na umri wa miaka sita na kuanza maisha katika klabu hiyo kama mshambuliaji , tayari akiweza kuonyesha umahiri wake na nidhamu swala lililomsaidia kukwea mlima wa ufanisi.
Fabian Taupin-:naibu kocha wa klabu ya Roissy-en-Brie: Alikuwa na tabia ya ujasiri . Alikuwa mchezaji mzuri lakini hakuwa mchezaji mzuri pekee kwa kuwa tulikuwa na mwaka mzuri wa wachezaji. Ungemwambia alipaswa kuwa katika klabu hiyo mwendo wa saa kumi na mbili alfajiri -yeye alifika katika klabu hiyo saa kumi na mbili kasorobo, alikuwa tayari saa kumi na moja na nusu, alikua anapatikana kila mara akitaka kusakata soka, Kila mara alitaka kuimarika zaidi, hakusita.
'
Iwapo angechezewa visivyo mara kadhaa , angelia'Paul Pogba na Mathias wakati wa mechi ya kitrafiki ya wakfu wa Juan Cuadrado
Mbali na masomo yake na kuichezea klabu ya Roissy, Pogba angetumia wakati wake mwingi akinoa makali yake katika uwanja wa City Stade, uwanja unaotumiwa kuandaa michezo tofauti uliopo karibu na nyumbani kwao mbali na kushiriki katika michezo ya kiwilaya pamoja na nduguye mkubwa.
ZakariaTimera: Alicheza pamoja na Pogba alipokuwa umri wa miaka 7: Paul alikuwa mwanafunzi mwenye nidhamu aliyefanya bidii shuleni, lakini hamu yake kuu ilikuwa soka. Wakati kulikuwa hakuna masomo , alipendelea kwenda katika uwanja wa City Stade mwendo wa saa saba kusakata soka. Tungesalia katika uwanja huo hadi sa mbili ama hata saa tatu usiku.
"Uwanja ulikuwa karibu na nyumba yetu, dakika chache tu .Mwanzo kitu ambacho kingetuzuia kutocheza ni iwapo tulikuwa na kiu kingi ambapo tungetoka kwenda kupata kinywaji na kurudi uwanjani .Kitu muhimu kabisa ilikuwa soka.
Aliivutia klabu ya Le Havre
Pogba huenda alivutia wengi alipokuwa akiichezea klabu yake ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 13 lakini hakuitwa katika kituo cha kufunza soka ya kitaifa cha Clairefontaine national football .
Hatahivyo, klabu inayocheza soka ya kulipwa ya Le Havre ilikuwa tayari imeanza kuchunguza kipaji cha mchezaji huyo kupitia klabu ya Torcy, ikamsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 14 katika shule ya kufunza soka.
Franck Sale, Mkuu wa kitengo cha usajili wa wachezaji katika klabu ya Le Havre: "Nilisikia kuhusu Pogba katika kitongoji cha Paris kutoka kwa wenzangu ambao walimuona wakati alipokuwa mdogo akiwa na umri wa kati ya miaka 11 na 12 , hivyobasi tulienda kumuona mara moja. Alikuwa akicheza katika uwanja wa City Stade tuliona ujuzi wake na baadaye tukaenda kuona akicheza katika uwanja mkubwa .Paul tayari alikuwa akicheza na vijana wakubwa. Kulikuwa na klabu nyingi zilizokuwa zikimhitaji lakini ni chache ambazo zilipata fursa kumuona akicheza. Tulimgundua mapema. Kwa kweli PSG ilimuona kwa sababu alikuwa katika vitongoji vya Paris.
Alipokuwa akiondoka nyumbani kwaolorentin na Mathias Pogba wajiunga na mama yao Yeo
Ilimchukua muda wa saa moja na nusu kwa Pogba kusafiri kutoka nyumbani kwao hadi makao makuu ya shule ya mafunzo ya soka kutoka Paris. Hatahivyo safari hiyo haikumkwaza kijana huyo ambaye alijawa na hisia alipokuwa uwanjani.
Sale: "ilikuwa vigumu kwake kwa kuwa alikuwa na ari ya kuwa mchezaji wa kulipwa na kwa sababu Paris na Havre haziko mbali. Angeweza kwenda nyumbani kwa urahisi na ilikuwa rahisi kwa familia yake kumtembelea , lakini alikuwa na malengo hadi hatuwezi kusema kwamba alivunjika moyo kwa kuiwacha familia yake -ilikuwa rahisi kwake.
'Tulimsukuma kufanya bidii zaidi'Paul Pogba alikuwa nahodha wa kikosi cha uFransa cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 16
Haikuwa rahisi kwa kiungo huyo wa kati katika klabu ya Le Havre. Pogba alikuwa na kipaji na ujasiri katika kazi yake , lakini wakufunzi wake walimtaka kufanya bidii zaidi ili kuafikia malengo yake ya ufanisi. Sale: "Alikuwa akifanya bidii sana lakini haikuwa rahisi kwa wakufunzi kwa sababu mara nyengine alionekana kuwa mjeuri. Tunazungumzia kuhusu hisia za kujiona muhimu mara nyengine ambazo bado zinaonekana katika tabia yake katika mechi fulani. Alikuwa na bidii lakini tulijua anaweza kujibiidisha zaidi na ndio maana tulimsukuma kufanya hivyo.
Alionekana nchini Scotland, akielekea Manchester United.Klabu ya Le havre ilipinga usajili wa Pogba uliofanywa na man United lakini mkataba huo uliidhinishwa Oktoba 2009
Pogba alivutia timu nyingi alipojiunga na timu ya taifa ya Ufaransa yenye wachezaji wasiozidi umri wa miaka 16. Mabingwa wa Itali Juventus, walikuwa na hamu naye kama vile Manchester United baada ya Pogba kuiwakilisha timu yake katika michuano ya vijana katika ziara ya Scotland. Pogba aliamua kujiunga na Man United huku Fifa ikiunga mkono mkataba huo mwezi Octoba 2009 baada ya mgogoro kati ya United na Le Havre kuhusu kandarasi yake.
Sale: "Nilikuwa tayari nimewaonya wakuu wangu kwamba ni hatari kuwawacha wachezaji wetu vijana kwenda katika zitra kwa kuwa vilabu vya Uingereza vinawachunguza sana. Nikiwa mtu niliyejua kuhusu kipaji chake, sikushangazwa hata kidogo kwamba Man United walikuwa wana hamu naye. Lakini kulikuwa na klabu nyengine nyingi ambazo zilikuwa zikimnyatia. Ilituvunja moyo sana kama wakufunzi , kwa sababu tulitaka kumuingiza katika timu ya wachezaji wa kulipwa . Wakati huo kandarasi yake ilikuwa wazi ndiposa United wakachukua fursa hiyo.
...

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post