DEAL DONE: KICHUYA ASAJILIWA SIMBA MSIMU HUU


Muda mchache baada ya Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ kusema hawatambuachia mchezaji wanayemtaka kuondoka, taarifa zinasema wamemalizana na Kichuya.

Kichuya alitakiwa kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini na tayari alimaliza mkataba na Simba. Lakini uongozi huo umefanikiwa kumalizana naye.

“Ataondoka kesho kwenda Kenya kuungana na kikosi ambacho kinashiriki michuano ya SportPesa Super Cup,” kilieleza chanzo.

Taarifa zinaeleza Kichuya amesaini mkataba wa miaka miwili, ingawa kuna chanzo kingine kimesema mkataba huo ni wa miaka mitatu.

Kichuya ni kati ya wachezaji wamekuwa na mafanikio makubwa na kikosi cha Simba tokea watue wakitokea Mtibwa Sugar.

Kasi yake nzurini kikosini humo kwa misimu miwili mfululizo, kumemfanya kuwa kipenzi cha Wanasimba.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post