Tumtegemee Vanessa kwenye midundo kama ya Michael Jackson

Staa wa Bongofleva Vanessa Mdee ni miongoni mwa mastaa ambao wanautambulisha vyema muziki wa Bongo Fleva kwa kuufikisha kimataifa kutokana na kufanya kolabo na wasanii mbalimbali kutokea nchi tofautitofauti.

Kupitia instagram story ya Vanessa Mdee amepost video ikimuonyesha akiwa na Producer Humberto Gatica kutokea Marekani ambaye alishawahi kuhusika kwenye ngoma tofauti za mastaa wakubwa akiwemo Marehemu Michael Jackson, Celine Dionna wengine wengi.
kutokana na Vanessa Mdee kuwa karibu na Producer huyo inaweza ikawa ni good news kwa mashabiki pengine Vanessa Mdee yuko mbioni kutoa ngoma mpya chini ya producer huyo ambaye ni legend katika muziki nchini Marekani.








Vanessa Mdee kwa sasa yupo London UK akifanya dili kubwa na kampuni na moja ya kampuni ambayo inasemekana kufanya naye kazi ni kampuni ya magari ya Bentley.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post