BILIONEA MPYA KUWEKEZA BILIONI 30 YANGA, ISHU KAMILI IKO HIVI



Kuna taarifa za chini chini zinazo sema kuwa kuna bilionea anayetaka kuwekeza bilioni 30 ndani ya klabu ya yanga, lakini bilionea huyo ameweka sharti kuwa ni lazima kwanza kufanyike mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo.

Yanga imepitia katika wakati mgumu baada ya aliye kuwa mwenyekiti wao Yusufu Manji kuachia ngazi ndani ya klabu hiyo.

Taarifa tulizo zipata ni kuwa yanga watafanya mikakati kumruhusu mwekezaji huyo mara baada ya mkutano mkuu wa klabu.

Tulipo mtafuta msemaji wa klabu Dismas Ten  alisema kuwa yeye sio mhusika wa jambo hilo na hizo habari sio za kweli, tulifanya jitihada ya kumtafuta Mkwasa kuzungumzia swala hilo hatukufanikiwa.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post