Wema Sepetu ni Maliasili ya Taifa – Idris Sultan


Baada ya kuvuja kwa picha na video zikimuonesha mrembo Wema Sepetu akiwa kwenye Swimming Pool, video ambazo zilizua gumzo mitandaoni wiki iliyopita. Hatimaye aliyewahi kuwa Boyfriend wake Idris Sultan amesema picha hizo aliziona na amechukulia kawaida.

Akiongea na waandishi wa habari Jumapili Aprili 01, 2018. Idris amesema kuwa Wema Sepetu ni maliasili ya taifa hivyo hakuna tatizo kama akiamua kuonesha mwili wake kwani watu wengi wanataka kuuona.

Idris alipoulizwa tukio la kuvuja kwa video hizo za Wema alilipokeaje? alijibu “Maliasili ya taifa i think ina haki ya kuoneshwa kwa wananchi wanaotaka kuiona”

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post