Baada ya Kifesi Kuacha Kazi Kwa Daimond Afunguka Kufanya kazi na Msanii Huyu


Aliyekuwa mpiga picha wa Diamond na WCB kwa ujumla, Kifesi amefunguka iwapo yupo tayari kufanya kazi na wasanii wengine Bongo.

Kifesi amesema yupo tayari kufanya kazi na msanii yeyote ila kazi hiyo isiendane kinyume na matakwa ya imani yake.

“Kama nilivyoelezea sasa hivi nitakuwa ni mfanyakazi huru, kujitegemea mimi kama mimi, nipo huru kufanya kazi na msanii yeyote lakini endapo ufanyaji kazi huo hautanihusisha kwenda kiyume na imani yangu,” Kifesi ameiambia Bongo5.

“Mimi bado ni mpiga picha naendelea na kazi yangu lakini nimeacha kufanya kazi na WCB lakini simaanishi nitaendelea kuwa mwajiriwa wa msanii,” ameongeza.

Mwishoni mwa weekend iliyopita March 30, 2018 Kifesi alitangaza kuacha kazi yake ndani ya WCB kwa kile alichodai kuwa anataka kujiari na kuwa karibu na Mungu wake.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post