Rais wa zamani wa Brazil Lula da Silva awasili jela kuanza kutumikia kifungo chake


Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amewasili katika jela la Curibita kuanza kutumikia kifungo cha miaka 12 jela baada ya siku ya Ijumaa, mahakama kumhukumu kwa mashitaka ya ufisadi.

Matangazo ya moja kwa moja ya vituo vya televisheni vya Brazil yameonesha akiwasili kwa helikopta katika makao makuu ya polisi katika mji wa Curibita ulioko kusini mwa Brazil.

Hayo yanajiri baada ya Lula da Silva kujisalimisha kwa polisi ambapo mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 72 aliondoka Sao Paoli akiwa amezingirwa na walinzi kwenye jengo la muungano wa wafuasi vyama mjini humo.

Lula alikutwa na hatia ya kupokea rushwa kutoka kwenye kampuni kubwa ya ujenzi, ili iweze kupata mikataba ya serikali.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post