Najuta: Mchepuko Anataka Kunipeleka Kwa Makonda


Ilikuwa kama utani mwaka 2013 tukiwa kwenye daladala za Kimara - Posta. Nilimtongoza akanitunuku na mimba ya mtoto wa kike ikapatika na akajifungua salama salmini.

Kifupi nimekuwa nikitoa huduma zote kwa huyu mchepuko tokea akiwa mjamzito na nahudumia kwa kutoa kama laki mbili na nusu kila mwezi, lakini haridhiki kabisa anasema fedha haitoshi sababu mtoto anaugua mara kwa mara na mimi nilishamwambia siwezi toa zaidi ya hapo coz hata wife hamjui na nina watoto wengine kwa wife.

Tatizo ni tokea Makonda atangaze kuwa wanawake waliotelekezewa watoto wakatoe taarifa, aisee the whole week am at high risk... nalala kwa shida ni mawazo tu hadi wife kanistukia.. Ni ananitishia kila siku simu haziishi kuwa jumatatu atakuwa wa kwanza kunireport kwa Makonda, na mzaramo huyu kichwa chake antena haipo sawa najua hatanii ataenda tu. Nimejaribu kumtumia rafiki yake amshauri imeshindika.

Jana jioni nimemtumia laki moja, asubuhi hii kanitumia sms... "Unajua kulea wewe? Umenitumia vihela vya mboga hivi huoni wanaume wenzio wanavyotoa? Unajua Mobetto anapewa sh ngapi kwa siku? Kwa taarifa yako hii ni nauli ya tax kesho kwenda kwa Makonda"...

Wakuu hapa nakaribia kuwa chizi sometime najikuta naongea alone. Ushauri tafadhali.

By Pius

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post