Anthony Joshua Noma Ashinda Pambano Lake na Joseph Parker Kwa Kishindo


Usiku wa April 1 2018 mashabiki wa mchezo wa ngumi duniani walikuwa wanasubiria kwa hamu pambano la mabondia Anthony Joshua na Joseph Parker kupanda ulingoni kila mmoja akitarajiwa kulinda rekodi yake.

Bondia Anthony Joshua leo amefanikiwa kumpiga Joseph Parker kwa ‘Unanimous Decision’ hilo likiwa ni pambano lake la 21 kwa Athony Joshua kushinda kati ya mapambano yake 21 ila ni pambano lake la kwanza kushinda kwa point ila yote 20 yaliyosalia amekuwa akishinda kwa‘Knock Out’

Kwa upande wa Joseph Parker mwenye umri wa miaka 26 akizidiwa na Anthony Joshua miaka miwili, yeye anapoteza pambano lake la kwanza kati ya mapambano yake 25 akiwa kashinda 18 kwa Knock Out, 6 kwa point, Joshua anazidi kudhihirisha ubora wake katika mchezo huo baada ya ushindi huo kumpa Ubingwa wa WBO

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post