Zlatan adhulumiwa na Baba, amfukuza Mino Raiola


Leo Beenhakker alisafiri mpaka kunako mji wa Malmo FF. Kabla ya safari ya Sweden akiwa ofisini kwake, mkurugenzi mkuu wa Ajax alifuatwa na mdenmark mmoja ajulikanae kama John Steen Olsen. Olsen alimshawishi Beenhakker kumchukua Zlatan. Fabio Capello nae alimmendea Zlatan alipokuwa kocha As Roma.
Maisha yake ya Ajax yalikuwa magumu kutokana na gharama za usajili wake kuwa mkubwa.
Alikabidhiwa jezi namba 9. Alibebeshwa heshima na sifa kedekede kwa mataraji kuwa angevaa viatu vya Marc Van Basten. Zlatan aliporudi hotelini aliona dunia nzima imemkabidhi jiwe kubwa mno. Alipatwa na wasiwasi mkubwa kwani alijiona mdogo sana na hakuwa mchezaji maarufu. Gumzo lilizuka sana katika miji mbalimbali nchini uholanzi; Watu walipigwa butwaa kwa mchezaji mdogo kuweka rekodi ya ununuzi ndani ya klabu.
Mkosi ulianza baada ya kutolewa na Celtic klabu bingwa. Tabu kubwa aliyokumbana nayo uholanzi ni lugha. Uliibuka mgogoro mkubwa baada ya kocha wake Bw. Co Adriaanse kumshutumu kwa utovu wa nidhan. Kiwango chake kiliporomoka mno. Mashabiki walikerwa na tabia zake.
Bodi ilipokea malalamiko mengi kutoka kwa wadau wa soka wakimtaka Zlatan afukuzwe.
Baada ya mchezo dhidi ya Groningen, Zlatan alifungiwa michezo mitano na chama cha soka uholanzi (KNVB) kwa kosa la kumpiga mchezaji mwenzake kiwiko. Kipindi cha majira ya baridi Zlatan alitaka kuondoka. Alimpigia simu mkurugenzi wa Hasser Borg akimtaka amtafutie klabu ya kwenda kucheza kwa mkopo.
Borg ndiye aliyefanya makubaliano wakati Zlatan anajiunga na Ajax.
Zlatan alimheshimu na kumwamini sana Borg kama baba yake na mambo mengi alimshirikisha.
Katika maisha lazima changamoto ziwepo. Kilichomkera zaidi Zlatan ni mshahara wake.
Alinunuliwa kwa gharama kubwa lakini yeye ni mmoja wa wachezaji waliokuwa wakilipwa mshahara kiduchu kikosini. Inasemekana kuna figisu ilifanywa katika makubaliano ya mkataba wake bila yeye kujua. Borg alifanya ujanja ujanja wote bila kumshirikisha Zlatan.
Siku moja Andre Bergdolmo alimpigia simu Zlatan na kumuomba wakapate chakula cha jioni. Andre alikuwa mchezaji wa Ajax. Alijua hali ya Zlatan na alifahamu wazi kuwa Zlatan alikuwa anajituma sana. Alimweleza ukweli wa dili lake lote.
Alimfahamisha jinsi Borge alivyomzunguka bila yeye kujua. Baada ya kuachana nae jioni ile Zlatan aliandika yafuatayo “Alijifanya yupo upande wangu, kumbe mnafiki tu, alitumia mgongo wangu kwa maslahi yake na kwa ajili ya klabu ya Malmo FF, na kila ninapowaza napatwa na ghadhabu sana. Kwanza hela kwangu sio kitu, ila ni kitu cha kuja na kuondoka, kunifanya mimi mjinga, na zwazwa ili kujinufaisha kunanitia uchizi”mwisho wa kunukuu.
Shida kubwa kwenye ufanisi wa Zlatan ilikuwa Hassan Mido ambaye aliaminiwa zaidi na mwalimu Adriaanse. Matokeo mabovu yalimuondosha Adriaanse na Ronald Koeman alikabidhiwa timu. Koeman alimpenda zaidi zlatan na hapo ndipo maisha mapya klabuni hapo yalianza.
Katika mchezo wa Fainali dhii ya Utrecht mpira uliisha dsakika 90 bila bila. Na ilibidi mchezo uende dakika 30 za nyongeza kwa mfumo wa goli la dhahabu. Dakika 3 tu mchezo kuanza kwenye zile dakika 30 Zlatan aliwainua Mashabiki wa Ajax baada ya kufunga goli murua kabisa na mchezo kuishia pale pale kwa Ajax kutwaa ubingwa wa kombe KNVB.
Siku moja baada ya mazoezi Zlatan alipokea simu ya mtu asiyemfahamu. Akajitambulisha kwa Jina la Mino Raiola. Akamweleza kuwa yeye ni wakala anahitaji kufanya nae kazi. Zlatan akamwambia sina muda wala asimsumbue kabisa. Zlatan hakuhutaji tena mtu wa karibu hasa kwenye masuala ya fedha kwani wote aliwaona wanadhulumu.
Raiola akaamua kumtafuta Maxwel ambaye alikuwa rafiku mkubwa wa Zlatan. Akamwagiza aongee nae kwa niaba yake. Maxwel akaenda chumba alichokuwa anakitumia Zlatan. Alimkuta Zlatan anacheza game. Akamwambia ana ujumbe wake.
Zlatan akauliza upi, Max akamwambia kuna wakala… kabla hajamalizia Zlatan akadakia mwambie sina muda aachane na mimi. Max alikuwa anamfahamu Zlatan vyema hakumsumbua sana aliacha barua ya mwaliko kwenye kochi. Barua ile ilitumwa na Raiola kwa lengo la kutaka wakutane kwenye hoteli ile. Kwenye barua ile iliambatanishwa vitu ambavyo vilimchanganya sana Zlatan.
.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post