Kiungo wa Simba Jonas Mkude ameumia kifundo cha mguu wa kulia (ankle) wakati wa mazoezi ya jioni ya klabu hiyo kwenye uwaja wa Boko Veterans, Dar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Njombe Mji.
Daktari wa Simba Yassin Gembe kupitia instagram account ya Simba amenukuliwa akisema amegundua majeraha ya Mkude sio makubwa sana na kutokana na anaendelea vizuri baada ya matibabu ya awali aliyompatia.
“Mkude ameumia kwenye kifundo cha mguu wa kulia, kwa vipimo vya awali sio majeraha makubwa sana ila kesho tutatoa taarifa kamili kuhusiana na hali yake kwa ujumla.”
“Kwa sasa napenda kusema anaendelea vizuri kutoka katika matibabu ya awali tuliyompatia.”
Afisa habari wa Simba Haji Manara pia ame-post taarifa iliyotoka kwa daktari Gembe kwamba Mkude huenda akawa nje ya uwanja kwa siku mbili hadi tatu.
“Kwa mujibu wa daktari wetu, injury ya Jonas ni ndigo. Anasema maximum anaweza kuwa nje kwa siku mbili hadi tatu, hii ndiyo taarifa rasmi ya klabu toka kwangu”-Haji Manara.
Tags
LIGI KUU VPL