Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 28.03.2018: Gabriel Jesus amekataa mshahara mpya, City wanamtaka Isco



Gabriel Jesus
Image captionGabriel Jesus amewaambia maafisa wa Ligi ya Primia na wale wa Brazil mkataba mpya ni mpaka msimu wa majira ya joto
Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus, mwenye umri wa miaka 20, amekataa malipo ya £90,000- kutoka kwa viongozi wa Ligi ya Primia na wale wa Brazil na hivyo watalazimika kusubiri hadi msimu wa majira ya joto kujadili mkataba mpya . (Mail)
Manchester City wanammezea mate mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya Uhispania ya Real Madrid Isco, mwenye umri wa miaka 25 ambaye wanataka kumnunua £75m msimu wa majira ya joto . (Sun)
Mlinzi wa Chelsea raia wa Uhispania Marcos Alonso, mwenye umri wa miaka 27, anasema bvado hajafikiria kuondoka the Blues huku kukiwa na uvumi juu ya hatma yake katika Stamford Bridge. (Marca)
Macho ya Everton sasa yameelekezwa kwa Shakhtar Donetsk meneja wa Ureno Paulo Fonseca, 45, kuchukua nafasi ya meneja wa sasa wa timu hiyo Sam Allardyce. Everton wanaaminiwa kumtaka kijana kuongoza timu yao. (Mirror)
Arsene Wenger
Image captionMeneja wa Arsenal Arsene Wenger ameikasirikia sana England kwa namna walivyoweza ''kummudu " mchezaji wa kiungo cha kati Jack Wilsher
Real Madrid wamenuwia kusaini mkataba na mlinda lango wa kimataifa wa Brazil ambaye kwa sasa anaichezea Roma Alisson, 25, msimu huu wa majira ya joto. (Marca - in Spanish)
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameikasirikia sana England kwa namna walivyoweza ''kummudu " mchezaji wa kiungo cha kati Jack Wilshere, mwenye umri wa miaka 26, wakati wake wa mechi za kimataifa. Wilshere alijeruhiwa lakini anatarajiwa kuwa fiti kukabiliana na Stoke wanaotarajia kutemebela Emirates Jumapili . (Star)
Mlinzi wa zamani wa Real Madrid Roberto Carlos anasema mshambuliaji wa Paris St-Germain mBrazil Neymar, mwenye umri wa miaka 26, alilazimika kuondoka Barcelona kwasababu ya Lionel Messi. (FranceFootball - in French).
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Barcelona mFrance Samuel Umtiti, mwenye umri wa miaka 24, alikataa kujibu swali kuhusu kujiunga kwake na Manchester United msimu wa majira ya joto alipokuwa akifanya mazungumzo na na Wakatalonia juu ya mkataba mpya. (Mirror)
James MaddisonHaki miliki ya pichaMAGNUM PHOTOS
Image captionTottenham, Chelsea, Everton na Manchester City kwa pamoja wameonyesha nia ya kusaini makataba na James Maddison msimu huu wa majira ya joto
England itakuwa na fursa moja tu ya kuchezea mpira rasmi wa Kombe la Dunia wa Adidas kabla ya mashindano ya msimu huu wa majira ya jotokwasababu ya mkataba wa kibiashara wa FA na Nike. (Times)
Norwich imeweka kiwango cha bei ya £25m kwa yeyote atakayetaka kumnunua mchezaji wake wa kiungo cha kati wa England 21 James Maddison, huku Tottenham, Chelsea, Everton na Manchester City kwa pamoja wakiwa na nia ya kusaini nae mkataba mnsimu huu wa majira ya joto. (Mirror)
Gabby AgbonlahorHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionGabby Agbonlahor amesema atakamilisha mwaka wa 17- wa uhusiano wake na kilabu cha Aston Villa msimu huu wa majira ya joto
Newcastle imekuwa ikimsaka mchezaji wa kiungo cha kati wa Besiktas Oguzhan Ozyakup, mwenye miaka 24, kwa mtizamo mpya wa kusaini mkataba wa bila malipo na Uturuki katika msimu wa majira ya joto. (Turkish-Football.com).
Mshambuliaji wa Aston Villa Gabby Agbonlahor, mwenye umri wa miaka 31, atakamilisha mwaka wake wa 17- wa uhusiano wake na kilabu hicho msimu huu wa majira ya joto, hata kama watapanda na kuingia Ligi ya Primia. (Telegraph)
Washiriki wa michuano ya kombe la klabu bingwa wanatarajia kumshitaki Afisa mkuu Sam Rush wakimtaka alipe £7m, kwa madai yanayohusiana na gharama za uhamisho na malipo ya mchezaji wakati wa uongozi wake katika kilabu. (Mail)

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post