Imebaki siku moja watanzania tuweze kushuhudia mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya Congo DRC, game ambayo itachezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Game ya Tanzania na Congo ni mchezo ambao upo katika kalenda ya FIFA, hivyo kwa timu zote mbili huu ni mchezo muhimu ambao utaweza kuwasogeza katika viwango vya FIFA kama mmoja kati yao akipata matoke chanya.
Congo wapo nafasi ya 39 katika viwango vya FIFA na Tanzania wapo nafasi ya 146, kocha wa Congo Ibenge ameeleza sababu za kuchagua kucheza na Tanzania ni kutokana na ukaribu wa nchi hizo hivyo hawakuona sababu za kwenda kucheza na mataifa ya mbali.
Tags
Michezo