Baada ya bodi ya Ligi kutangaza kuahirisha michezo kadhaa ya Ligi Kuu wiki kadhaa zilizopita, leo afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura leo ametangaza ratiba mpya ya Ligi Kuu Tanzania bara hadi msimu unapomalizika.
Wambura ametangaza mabadiliko na ratiba ya game mbalimbali huku akieleza kuwa wanatazamia kuona ratiba ya CAF kwa Yanga kama ataingia hatua ya Makundi ndio watajua kama watafanya tena mabadiliko, mchezo wa Simba dhidi ya Yanga uliokuwa uchezwe April 7 umesogezwa mbele hadi April 29.
Tags
Michezo