Klabu ya Simba Yapewa Agizo na Rais


Wachezaji wa Klabu ya Simba imeagizwa kufanya vizuri katika mechi zake anazoendelea kucheza ili iwe njia moja ya wapo ya kumuenzi mchezaji wao wa zamani Mzee Arthur Mambeta aliyefariki jana (Marchi mosi, 2018) Jijini Dar es Salaam.

Agizo hilo limetolewa na maarufu kama 'Try again' wakati alipokuwa anazungumzia jinsi walivyoguswa na taarifa za msiba wa nyota wao zamani kama viongozi wa klabu hiyo.

"Marehemu Mambeta ni hazina ambayo Mungu ametupatia lakini sasa Mwenyezi Mungu mwenyewe amepitisha rehema yake kwa hivyo sisi kama Klabu ya Simba kwa masikitiko makubwa tunawaomba wanachama wetu na wapenzi wa wekundu msimbazi tumuenzi mzee huyu", amesema Salim.

Pamoja na hayo, Salim ameendelea kwa kusema "wachezaji wetu wafanye vizuri  katika mechi zinazokuja ili kumuenzi shujaa wetu huyu kwani ni moja ya wazee wachache waliokuwa wamebaki katika tasnii hii kwa wazee ambao walifanya vizuri na kuitendea mema klabu".

Nyota huyo wa zamani wa Simba, Mzee Arthur Mambeta anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumamosi (Machi 3, 2018) katika makaburi ya maeneo ya Buguruni Jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post