Yanga ipo tayari kwa ‘vigogo’ wa Al Merreikh

Mwenyekiti wa kamati ya mashindano Yanga Hussein Nyika amesema timu yao ipo tayari kupambana na wapinzani wao Township Rollers ya Botswana kwenye mchezo wa Caf Champions League hatua ya kwanza.

Nyika amesema kocha mkuu wa Yanga anaifahamu Township Rollers na watatumia mechi zao za ligi pamoja na michuano ya FA Cup kama maandalizi kuelekea mchezo huo.

“Tumepokea vizuri taarifa hiyo kwa sababu ndio timu ambayo tutakutana nayo kwa bahati nzuri tumewahi kuiona kwenye mashindano ilikuwa ikiheza na Kaizer Chiefs miaka miwili iliyopita.”

“Ni timu nzuri kwa sababu ni timu ambayo imeiondoa Al Merreikh, kwa hiyo mwalimu ameshajua anakutana na timu ya aina gani na kutokana na ratiba kubana, mwalimu atatumia mechi za ligi na kombe la FA kutengeneza kikosi chake ili kufanikisha malengo yetu.”

“Nimejaribu kuwasiliana na mwalimu amesema anaifahamu hiyo timu kwamba ni nzuri. Kinachotuumiza sisi ni majeruhi lakini mwalimu ameahidi kuwatumia wachezaji alionao kwa ajili ya kupambana na hiyo timu kufika hatua ya makundi na hicho ndio tunachokihitaji.”

“Niwaambie watanzania waendelee kuiunga mkono timu yao kwenye mashindano haya ili kufikia malengo na hilo linaweza kutimia kama tukiwa pamoja.”

Township Rollers imeitoa Al Merreikh kwa jumla ya magoli 4-2, mchezo wa kwanza uliochezwa Botswana Township ilishinda 3-0 lakini mchezo wa marudiano uliochezwa Sudan Al Merreikh ikashinds 2-1 na kufanikiwa kusonga mbele.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post