Tatizo la Pobga na Mourinho sasa kuchukua Sura Mpya na Hatma ya MAN U

Tatizo sio Pogba, kama Mouriho hatapata tiba ya magonjwa haya 3 baasi United wataangamia tu

Gumzo kubwa duniani kwa sasa ni kuhusu Paul Pogba, wachambuzi mbali mbali wamekuwa wakiongelea kiwango cha Mfaransa huyo ambacho katika siku za karibuni kinaonekana kupanda na kushuka.

Wakati Paul akinunuliwa kutoka Juventus iliaminika anakuja United kuwa mtawala mpya lakini kwa sasa Jose Mourinho anaonekana kuondoa fikra za wengi kwamba Paul atakuwa mfalme mpya katika klabu ya United.

Mengi yanasemwa na wengine wanasema Pogba ndio anayeiangusha Manchester United japo ukiangalia kwa nje ya box utagundua kwamba Pogba anatolewa tu kafara lakini yapo matatizo makubwa sana United.

1.Nemanja Matic, wapo wanaoona lakini wanajaribu kumficha kupitia kivuli cha Paul Pogba, uwezo wa Nemanja Matic wa sasa sio uwezo wa Nemanja Matic yule wa mwanzo wa msimu huu wa ligi.

Kiwango cha Matic kimeshuka sana, ukabaji, upandishaji timu na anaonekana kama amechoka na hii imeondoa balance katika timu tofauti na ilivyokuwa mwanzo na kumfanya Pogba abebeshwe mzigo mkubwa zaidi.

Wakati ligi inaanza Matic alikuwa akiongoza kwa kufanya tackling katika EPL lakini kwa sasa rekodi ya Mserbia huyo inashuka sana na anaonekana kupunguza sana tackling anazofanya uwanjani na mashabiki wa Chelsea wengi washaanza kuelewa kwa nini Cinte hakumng’ang’ania.

Wakati kiungo wa klabu ya Leicester City Wilfred Ndidi akiwa kileleni ambapo hadi sasa amefanya tackling 74, Nemanja Matic hadi sasa amefanya tackling 30(pungufu ya tackling 34)na akipitwa hadi na Ngolo Kante mwenye tackling 54.

2.Ulinzi, tatizo kubwa sana kwa United liko hapa na hili linaonekana hata kama sio mfuatiliaji wa soka unaweza kuona ugonjwa mkubwa kwa Manchester United, wana ulinzi dhaifu sana na hawako salama.

Timu nyingi ambazo Jose Mourinho amekuwa akifanya vyema na kushinda makombe amekuwa akijaribu kuzitengeneza kupitia eneo la ulinzi, na walinzi wakimuangusha huwa ndio anguko la Mourinho.

Msimu wakati unaanza United walionekana wa moto kutokana na eneo lao la ulinzi lilivyokuwa Eric Bailly, Marcos Rojo walionekana kucheza vizuri sana na matatizo yalianza walipopotea haswa Bailly.

Chris Smalling na Phill Jones ni wale wale, hawajawahi kuwa walinzi imara, sahau kuhusu Tottenham walivyotumia sekunde 11 kuwaua United na sahau pia kuhusu Newcastle lakini Sevilla wamethibitisha jinsi United walivyo na mabeki wabovu.

Sevilla walipiga mashuti mara 4 zaidi ya mashuti waliyopiga Manchester United na kati ya hayo 13 yalipigwa ndani ya eneo la box huku mashuti 8 yakilenga goli la United, na sasa De Gea anaonekana bora sana kutokana na mabeki wake kupwaya.


3.Ushambuliaji, wakati EPL inaanza United walifunga mabao 21 katika mechi 7 za mwanzo ikiwa ni wastani wa mabao 3 kwa kila mchezo lakini baada ya mechi 20 United wakawa wamefunga mabao 30 wastani wa 1.5 kwa kila mechi.

Mourinho anaonekana kutokuwa na mbinu mbadala kuhusu ushambuliaji na mara nyingi washambuliaji wanaonekana kufanya juhudi binafsi tofauti na City ambao wanaonekana kufanya mashambulizi yaliyopangwa.

Romelu Lukaku anaiangusha zaidi United amekuwa anaonekana mzito siku hadi siku, ana mabao 12 hadi sasa, mwanzo wa ligi alionekana hatari lakini mechi 19 za mwisho za EPL Lukaku ana mabao 5 tu.

United wanayumba na wanaweza kuanguka zaidi kama Mourinho hatatafuta tiba mbadala ya ulinzi ambao pembeni una walinzi wenye miaka 30+, kama hataacha kutafta tiba ya Matic na kama ataendelea kumlea Lukaku, Mou aachane na Pogba kwa sasa atibu hizo shida kubwa.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post