Real Madrid walivyopoteza point mbili dakika ya 89


Club ya Real Madrid ya Hispania usiku wa February 3 2018 imedhihirisha kuwa sasa ni rasmi haipo katika mbio za kuwania Ubingwa wa LaLiga, hivyo inapambania kumaliza katika nafasi mbili za juu hiyo ni baada ya sare yao ya 2-2 dhidi ya Levante.

Real Madrid ambao walikuwa ugenini dhidi ya wenyeji wao Levante katika uwanja wa Ciutat de Valencia wao ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 11 kupitia kwa Sergio Ramos lakini Levante wakasawazisha goli hilo dakika ya 42 kupitia kwa Boateng.

Game ilizidi kuwa ngumu zaidi kipindi cha pili licha ya kuwa Real Madrid walikuwa wanamiliki mpira kwa kiasi kikubwa, kwani baada ya kufanikiwa kupata goli la pili dakika ya 81 kupitia kwa Isco, furaha yao iliharibika dakika moja kabla ya game kuisha pale Pazzin alipoiswazishia Levante.

Real Madrid kwa sasa hawapo katika mbio za Ubingwa wa LaLiga baada ya FC Barcelona anayeongoza Ligi kumuacha Real Madrid mwenye point 39 kwa tofauti ya point 18, mchezo wa leo unakuwa ni mchezo wa nne kwa Real Madrid kutopata ushindi katika game zake sita za LaLiga alizocheza hivi karibuni kwani ameshinda mbili pekee.

Manara baada ya Yanga kupata penati “Baadhi ya maamuzi ni kichefuchefu”

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post