Mwamuzi Aliyetakiwa Achezeshe Mechi ya Azam, Simba Abadilishwa

Mwamuzi Aliyetakiwa Achezeshe Mechi ya Azam, Simba Abadirishwa


Mwamuzi Jonesia Lukyaa aliyekuwa achezeshe mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Azam FC, amebadilishwa.


Simba na Azam FC ambazo zinachuana kileleni mwa Ligi Kuu Bara, zinavaana kesho katika mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini.

Taarifa zinaeleza mwamuzi huyo mwanamama mwenye beji ya Fifa amebadilishwa na nafasi yake amepewa mwamuzi mwingine.

“Nafasi yake amepewa Emmanuel Mwandengwa, hivyo hatachezesha,” kilieleza chanzo.
Hata hivyo, hakukuwa na ufafanuzi kuhusiana na suala hilo la uamuzi wa kumbadili siku chache kabla ya mechi.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post