Baada ya Birthday Neymar aachwa


Baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa siku ya jana alipotimiza miaka 26, nyota wa PSG Neymar J ameachwa kwenye kikosi cha timu hiyo kilichosafiri kuivaa Sochuax kwenye mechi ya Kombe la Ufaransa.


Kocha wa PSG Unai Emery amesema amempumzisha Neymar kutokana na baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi kurejea kikosini akiwemo nyota Kylian Mbappe ambaye alikuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu.
Kocha Emery alikuwa ni miongoni wageni waliohudhuria sherehe ya kuzaliwa ya Neymar usiku wa jumapili na alilazimika kuondoka kwenye 'party' hiyo usiku wa manane baada ya tukio la kukata keki ili kwenda kupumzika kwaajili ya maandalizi ya safari.
Mchezaji aliyerejea kikosini ni kiungo Thiago Motta baada ya kuwa nje kwa mwezi mmoja kutokana na kuumia misuli huku mchezaji aliyesajiliwa kwenye dirisha la Januari Lassana Diarra naye amejumuishwa kikosini.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post