Idadi ya wanawake aliyotembea nao Idris yamtisha

Mchekeshaji wa filamu na muigizaji wa bongo 'movie' nchini Idris Sultan amesema hawezi kuweka bayana idadi ya wanawake aliyeweza kuwa nao katika mahusiano mpaka sasa kwa madai akiweka wazi anaweza akakosa mwanamke wa kumuoa.
 
Mchekeshaji wa filamu na muigizaji wa bongo 'movie' nchini Idris Sultan.

Idris amebainisha hayo kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kwenye ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni wakati alipokuwa akijibu swali la moja ya mashabiki zake aliyefahamika kwa jina la Mussa ambaye alitaka kufahamu idadi ya wanawake aliyotembea nao mchekeshaji huyo kabla hajawa maarufu mpaka sasa. 

"Nakumbuka idadi ya wanawake niliotembea nao lakini sidhani kama ntaweza kusema kiukweli, hili suala nikilizungumzia litaniondolea kabisa dalili na hatua zote ninazoweza mimi kupata mke au mwanamke. Hili suala hapana kwa sababu hakuna mwanamke yeyote atakae weza kunielewa baada ya kulisikia. Ila mimi ni mtoto mzuri", amesema Idriss.

Kwa upande mwingine, Idriss amesema sifa kubwa anayoangalia kwa mwanamke ambaye anataka kuwa ni yae ni lazima awe 'fiti'.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post