Mlinzi wa kushoto wa zamani wa Manchester United na Juventus Patrice Evra huenda akarejea nchini England baada ya kuwepo kwa tetesi za kutaka kusajiliwa na klabu ya West Ham United.
Evra ambaye kwasasa ni mchezaji huru baada ya kutimuliwa na klabu ya Marseille kwa kosa la kumpiga shabiki kwa madai ya kumdhalilisha, kitendo ambacho kilipelekea kufungiwa kushiriki mashindano ya Ualya hadi June 2018.
Evra na kocha wa sasa wa West Ham David Moyes wamewahi kufanya kazi pamoja ndani ya Manchester United msimu wa 2013 - 2014 kabla ya Evra kutua Juventus.
Tags
Michezo