Wanapenda Kuona Mauno Yangu Kama Nini- Snura

Mwanamuziki Snura Mushi ' SnuSexy' yeye amekiri kwamba tayari alikwisha jipanga kukabiliana na mabadiliko ya serikali haswa katika kuzingatia sheria za mavazi pamoja na maneno kwenye nyimbo zake baada ya kuletewa shida kwenye wimbo wake wa Majanga.


Akizungumza na www.eatv.tv Snura amesema kwamba ameamua kubadilika na jinsi sheria inavyotaka ndiyo maana kuanzia video zake mpaka mavazi ya kufanyia show yamebadilika na wakati mwingine huwa anafanya uhakiki wa maneno yake kwa kuwauliza wahusika ili asipate matatizo.

Snura amesema kwamba wasanii wote wanatakiwa kujipanga kwa mabadiliko hayo ya sheria na kuwasisitiza kwamba sheria hizo hazijanza leo wala jana bali zilikuwepo tangu zamani na wahusika walikuwa wakizifungia macho ila sasa wameamua kuziangalia

"Mimi nilijua hivi vitu vitatokea baada ya kupata shida kwenye chura, maana nilipofika kule kila kipengele nilichokuwa naoneshwa kilionesha wazi nilikosea. Hivyo niwaombe wasanii wenzangu waweze kujipanga kwa hili na tuweze kufuata sheria kama jinsi ambavyo zinataka". Snura

Akiongeza Snura amesema kwama "Mashabiki pia inabidi wakubali mabadiko na matokeo ya kumuona Snura na nguo ndefu kwenye video ikiwa ni pamoja na kutoona viuno vikikatwa  maana na wao wanapenda kuona miuno kwenye video kama nini. Mashabiki waking'ang'ania kutuona kama zamani wataua muziki wetu"

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post