Mkuu wa polisi amesema kwamba mashtaka yaliwekwa kama onyo kwa vijana wengine wanaosmabasza picha za ngono
Zaidi ya vijana 1,000 wameshtakiwa na polisi Denmark kwa kusambaza picha na video za ngono.
Wameshtakiwa kwa kutumia mtandao wa jamii wa Facebook Messenger kusambaza vipande vya video vilivyoonesha vijana wawili wenye miaka 15 wakifanya mapenzi.
Polisi wamesema kwa sababu vijana hao walikuwa wenye umri chini ya miaka 18, mashtaka yanaweza ongezeka hadi kosa la kusambaza picha zisizo ma maadili ya watoto.
Kampuni ya Facebook iliwataarifu mamlaka wa Marekani ambao walitoa taarifa kwa polisi Denmark.
Kama wakipatikana na hatia ya kusambaza picha zisizo na maadili kwa watoto, watawekwa kwenye orodha ya wadhalilishaji wa watoto kingono kwa miaka 10.
Vijana elfu moja na nne wanamashtaka nchi nzima ikiwa ni baada ya kusambaza picha na video kwa kutumia app hiyo ya kutuma ujumbe mwishoni wa mwaka jana.
Baadhi ya watuhumiwa wenye umri juu ya miaka 18 waliitwa katika vituo vya polisi kuhojiwa.
Watuhumiwa chini ya miaka 18 walipashwa habari kupitia wazazi wao.
Mkuu wa polisi wa Denmark amesema mashtaka hayo ni kama onyo kwa vijana kuthubutu kutuma video za ngono.
Yeyote atakayepatwa na hatia na mashtaka hayo anaweza kupata kifungo cha siku 20.
Kumekuwa na wito kwa serikali ya Denmark kuchukua hatua zaidi kuzuia picha za ngono ili kulipa kisasi.