Sio Sanchez tuu, hata hawa wamecheza chini ya Mourinho na Guardiola

Leo kuna uwezekano mkubwa dili la Alexis Sanchez kwenda Manchester United kutoka Arsenal kukamilika, kama dili hii ikikamilika Sanchez atakuwa amecheza chini ya makocha wawili wakubwa EPL Pep Gurdiola na Jose Mourinho.

Kumbuka Alexis Sanchez kabla ya kwenda Arsenal, aliuzwa na Pep Gurdiola akitokea Barcelona lakini Sanchez hatakuwa mchezaji wa kwanza kucheza chini ya makocha hao wawili, wapo hawa nyota wengine.

 Xabi Alonso, kwa misimu mitatu Xabi Alonso aliitumikia Real Madrid chini ya Mourinho lakini kipindi chote hicho Pep alitamani kumnunua Alonso na alipofika Bayern Munich mwaka 2014 alimvuta Xabi Alonso.

Zlatan Ibrahimovich, hii ni mara ya pili kwa Ibrahimovich kuwa chini ya Mourinho, mara ya kwanza ilikuwa Inter Milan lakini Zlatan pia alicheza chini ya Pep Gurdiola mwaka 2009 akiwa Barcelona na uhusiano wao inatajwa kuwa ulivurugika hapo.

Cesc Fabregas, wakati Fabregas akitoka Arsenal iliaminika kwamba anakwenda kuwa Xavi mpya ndani ya Barcelona lakini msimu wake mmoja tu ndani ya Barcelona ulibuma na baadaye Pep Gurdiola alimuuza kwenda Chelsea akakutana na Jose Mourinho.

Kevin De Bruyne, kati ya wachezaji ambao watu wa Chelsea wanamlaumu sana Jose Mourinho ni Kelvin De Bruyne, Mourinho hakuelewa uwezo wa Mbelgiji huyu na haikuwa kazi kwake kumuacha aende Ujerumani lakini baadaye Man City waliamua kumrudisha na sasa yuko chini ya Pep Gurdiola.

Pedro, hadithi ya Pedro na ya Fabregas zinafanana fanana kwani Pep Gurdiola ndiye alitoa ruhusa kwa Pedro kuondoka Barcelona ambapo aliitumikia tangu akiwa na timh B nyota huyo alikwenda Chelsea kukutana na Jose Mourinho.

Samuel Etoo, kama ilivyo kwa Zlatan Ibrahimovich, huyu naye alicheza chini ya Mourinho mara mbili akiwa na Inter na pia Chelsea lakini pia nyota huyu wa Cameroon amewahi kucheza chini ya Pep Gurdiola alipouzwa kwenda Barcelona.

Maxwell, alipokuwa Inter alikuwa chaguo la kwanza la Jose Mourinho katika beki ya kushoto lakini baada ya msimu mmoja tu Maxwell alivutiwa na kwenda Barcelona kwenda kucheza chini ya Pep Gurdiola.

Claudio Pizzaro, wakati Jose Mourinho akikaribia kuondoka Chelsea mwaka 2007 huu ulikuwa usajili wake wa mwisho mwisho lakini baada ya kucheza sana soka mwishowe Pizzaro aliamua kujiunga na Bayern Munich chini ya Pep Gurdiola

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post