Siamini Madrid bila Ronaldo - Zidane


Baada ya kuwepo kwa habari nyingi kuhusu Ronaldo kutaka kuondoka Real Madrid, hatimaye kocha wa mabingwa hao wa Hispania Zinedine Zidane amesema nyota huyo hataondoka.
''Ronaldo kuondoka Madrid ni jambo la kufikirika, siwezi kuifikiria Real Madrid bila Ronaldo, lakini nina uhakika kuwa mpango wa Ronaldo ni kumalizia soka ndani ya klabu hii'', amesema Zidane mchana huu mbele ya wanahabari kuelekea mchezo wa La Liga dhidi ya Celta Vigo.
Zidane amelazimika kuongelea suala hilo baada ya siku za hivi karibuni kuwepo kwa taarifa kuwa nyota huyo wa Ureno anashinikiza kupatiwa mshahara mnono utakao mfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani tofauti na hivi sasa ambapo anazidiwa na mpinzani wake Lionel Messi pamoja na Neymar Jr.
Ronaldo mwenye miaka 32 ambaye pia ni mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo alisaini mkataba mpya mwaka 2016 unaomweka klabuni hapo hadi mwaka 2011.
Mkataba huo ulimfanya kuwa mwanasoka mwenye mshahara mnono zaidi kabla ya Neymar kusaini mkataba mnono na PSG, uliomfanya kuwa juu ya wote Ronaldo na Messi. Messi amesaini mkataba mpya mwaka 2017 ambao umemfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi.
Real Madrid itacheza na Celta Vigo kesho mchezo wa La Liga ambapo hadi sasa mabingwa hao watetezi wana alama 31 katika nafasi ya nne, wakizidiwa alama 11 na vinara Barcelona wenye alama 14.
 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post