Tito Onesmo Machibya
anayejulikana kama 'Nabii' Tito (44) ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nong'ona
Manispaa ya Dodoma leo Januari 29, 2018 amepandishwa mahakamani katika mahakama
ya wilaya kwa shtaka la kutaka kujiua.
Nabii Tito amepandishwa kizimbani
leo akidaiwa kutaka kujiua mwishoni mwa wiki jana ambapo alijichana chana na
wembe katika baadhi ya maeneo ya mwili wake wakati Jeshi la Polisi likifanya
uchunguzi nyumbani kwake.
Januari 23, 2018 Nabii Titoo
alikamatwa na jeshi la polisi akituhumiwa kufanya uchochezi na baadaye
alipelekwa kupimwa akili katika hospitali ya wagonjwa wa akili (Mirembe) na
kufahamika kuwa mtu huyo alikuwa na matatizo ya akili, hivyo jeshi la polisi
liliendelea kumshikilia kwa ajili ya usalama wake na siku jeshi hilo
lilipokwenda kufanya uchunguzi nyumbani kwake ndipo alifanya jaribio la kutaka
kujiua.
Tags
kitaifa