Msimamo wa Kagera Sugar baada Nyosso kutoka kwa dhamana


Baada ya beki wa Kagera Sugar Juma Nyosso kuachiwa huru kwa dhamana kutokana na kushikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumpiga shabiki wa soka katika uwanja wa Kaitaba Bukoba baada ya game ya Simba dhidi ya Kagera Sugar kumalizika kwa Simba kupata ushindi wa magoli 2-0, leo umetoka msimamo wa Kagera Sugar.

Juma Nyosso anatuhumiwa kutenda kosa hilo baada ya mchezo na baadhi ya mashuhuda walisema kuwa Nyosso alimpiga shabiki baada ya kutolewa maneno yasiofaa na kupigigiwa vuvuzela masikioni, mratibu wa Kagera SugarMohamed Hussein amenukuliwa na shaffihdauda.co.tz akifafanua msimamo wa club baada ya Nyosso kutoka kwa dhamana.

“Jambo hili sisi tunaliangalia kwa macho mawili, kwanza tuweke wazi msimamo wetu, sisi hatutompa adhabu yoyote Nyoso kwa sababu yule shabiki alimkosea mchezaji wetu pamoja na Nyoso kuonekana kuwa na tabia ya ukorofi lakini kwa hili yule shabiki alimkosea na mimi nilishuhudia.”>>> Mohamed Hussein

“Kumpulizia mtu vuvuzela kwenye sikio haikuwa sawa lakini wakati huo mchezaji ndio ametoka uwanjani kucheza, lakini shabiki huyo alikuwa akimshabulia Nyoso kwa matusi hata wakati mchezo unaendelea na wakati wa mapumziko bado aliendelea kumtukana sasa na yeye ni binadamu alighadhabika.”>>>Mohamed Hussein

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post