BURUDANI
Lady Jaydee aeleza sababu ya nyimbo zake kutochezwa Clouds
By
|
Lady Jaydee ameeleza kuhusu nyimbo zake kushindwa kuchezwa Clouds Media wakati ilionekana tayari wameshamaliza bifu lao.
Akiongea na Dizzim Online msanii huyo amesema, hajawahi kukataza nyimbo zake kuchezwa na kituo hicho hata hivyo walisharuhusiwa na Seven lakini hakuna kilichofanyika.
“Ilisemekana kuwa mimi ndio nilikataza nyimbo zangu kupigwa, jambo ambalo sio kweli. Mimi sikukataza nyimbo zangu kupigwa na hakuna sehemu yoyote niliyoandika nyimbo zangu zisipigwe, wao ndio waliamua kwa sababu kuongea kwangu kule kwamba nyimbo zisipigwe. Baada ya hapo walisema akitoa ruhusa nyimbo zake zipigwe zitapigwa. Seven aliongea na akatoa Go ahead je walipiga? Kwa hiyo hapo sio tatizo langu mimi, hapo inadhihirika wazi kabisa kuwa tatizo liko wapi na mtu anaweza kuongea kitu sio kwa kumaanisha,” amesema Jide.
Mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2016 Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alipokuwa akiongea na kipindi cha XXL alisema, “Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige, jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tukikutana, nimuombe tena [Lady Jaydee] kama tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu.”
Tags
Udaku