YANGA yakwea Pipa kuifata MBAO FC

Dar es Salaam. Kikosi cha Yanga kimeondoka mchana huu kwenda jijini Mwanza ambako inakabiliwa na mchezo mgumu wa Mbao FC Jumapili.

Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa jijini Mwanza  ambapo wameahidi kuipa sapoti timu yao ili kuhakikisha inaibuka na ushindi kwenye mechi hiyo.

Mwenyekiti wa Mashabiki wa Mbao FC mkoani Mwanza, Mustafa Rajabu alisema wao wamejipanga vyema kuishangilia timu yao na wanaamini Yanga hawatoki na pointi Jumapili.

Yanga wanatarajiwa kutua Mwanza mchana huu ambapo wamesafiri kwa kutumia usafiri wa ndege tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post