Wekundu wa Msimbazi
Simba Jumamosi ya December 30 walikuwa
Nangwanda Mtwara kucheza mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji wao
Ndanda FC wanakuchele,
Simba wakiwa
Mtwara walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-0.

Niyonzima
Magoli ya
Simba yote mawili yalifungwa na
John Bocco dakika ya 52 na dakika ya 56, baada ya ushindi huo, kiungo wa
Simba raia wa
Rwanda Haruna Niyonzima ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa majeruhi alitumia ukurasa wake wa instagram kueleza furaha yake hasa uwezo wa
Bocco aliouonesha.
“Alhamudulilah kwa ushindi wa leo
na pia ongera sanaa wachezaji wote,kiukweli siku ya leo imekuwa siku
nzuri yenye furaha na amani,big up my brother Bocco Mungu azidi
kukusimamiya mwanangu.Simba nguvu moja
najua wataelewa one day”>>>Niyonzima