Nape ala Krismasi na Majonzi ya msiba



Wakati watu wengi wakisheherekea sikukuu hii kwa furaha lakini sio siku nzuri kwa Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye ambaye amefiwa na rafiki yake pia Kada wa CCM namba moja jimboni kwake ambaye alimsaidia kwa kiasi kikubwa katika kampeni zake za kuusaka Ubunge kwenye uchaguzi mkubwa wa mwaka 2015.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter amethibisha hilo kwa kuandika “Nakulilia kaka yangu Mayage! Nilizunguka nawewe ziarani nikiwa Mwenezi, nilijifunza mengi sana kwako! Pumzika kwa amani kada wa kweli wa CCM na mkweli sana, hata pale ukweli unapouma! Binafsi natambua mchango wako! RIP!“.

Mungu akupe nguvu Mhe. Nnauye katika kipindi hiki kigumu kwa kuondokewa na moja ya makada wakubwa wa Chama chako.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post