Mwanafunzi Aliyepiga Picha za Nyufa za Mabweni ya UDSM Apelekwa Kituo Kikubwa Polisi 'Central'

Mwanafunzi Aliyepiga Picha za Nyufa za Mabweni ya UDSM Apelekwa Kituo Kikubwa Polisi 'Central'


Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kumbusho Dawson amehamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi akitokea Oysterbay alikokwenda kuripoti.

Dawson alikwenda kuripoti Kituo cha Polisi Oysterbay leo Jumanne Desemba 5,2017 baada ya kuachiwa kwa dhamana jana usiku.

Mwanafunzi huyo ambaye ni mbunge wa serikali ya wanafunzi (Daruso) jana Jumatatu Desemba 4,2017 mchana alikamatwa na polisi akituhumiwa kusambaza picha kuonyesha nyufa kwenye majengo ya hosteli za UDSM.

Akizungumza na MCL Digital Makamu wa Rais wa Daruso, Anastazia Anthony alisema Dawson alikamatwa saa saba mchana na kupelekwa kituo cha polisi cha Chuo Kikuu kwa ajili ya kuhojiwa lakini ilipofika saa tisa alasiri polisi walisema hawana uwezo wa kumuhoji hivyo walimpeleka Oysterbay.
Chanzo: Mwananchi 

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post