Mtoto wa Grace Mugabe anatuhumiwa kumpa mimba mwanafunzi na kumlazimisha aitoe

Mwanafunzi wa miaka 22 nchini Afrika Kusini amemtuhumu Mtoto wa mke wa Rais Mstaafu wa Zimbabwe Grace Mugabe, Russell Goreraza kuwa amempa ujauzito na kisha kumgeuka na kumlazimisha autoe ujauzito huo.
Taarifa kutoka gazeti la serikali nchini Afrika Kusini zinaeleza kuwa binti huyo ambaye amejitambulisha kwa jina la Dineo Gwendoline Kekana ameeleza kuwa walianza mahusiano

December 2016 na kijana huyo na pindi tu alipomwamba ana mimba ndipo Russell alipoanza kutopokea simu za binti huyo na baadae kumwambia aitoe.
Hata hivyo taarifa kutoka Zimbabwe kwenye tovuti moja wapo ya habari zinaeleza kuwa Rusell amenukuliwa akisema kuwa hataki kusikia lolote kuhusu binti huyo, na kwamba hawezi kufanywa lolote, yeye sio Mwafrika Kusini na wala yeye sio raia wa nchi hiyo na anaweza asirudi tena nchini humo.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post