Shamsa Ford Akoshwa na Ya Dkt Shika Awataka Wasanii Kuiga Mfano Wake


Shamsa Ford Akoshwa na Ya Dkt Shika Awataka  Wasanii Kuiga Mfano Wake

Msanii wa Filamu Bongo, Shamsa Ford ameonyesha kufurahishwa kwa namna Dkt.  Louis Shika alivyokuwa maarufu kwa kipindi kifupi bila kutumia nguvu kubwa.
Katika hilo Shamsa amewataka wasanii wenzake kuinga mfano huo kwa kufanya kazi kwa bidii na zenye ubora na wakati wao ukifika watatoka tu na si vinginevyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shamsa ameandika;

Nilichojifunza kutoka kwa Dk. SHIKA Wasanii wengi hutumia nguvu kubwa ili wawe midomoni mwa watu, hufikia hatua ya kutengeneza skendo, kuunda mabifu, kuloga, kutukanana n.k.

Kuibuka kwa Dr. Shika kumefanya nijue kama umepangiwa kuwa maarufu utakuwa tu. Unadhani kusema tu ‘900 itapendeza’ ndio kunaweza kumfanya mtu awe maarufu? Hapana!, ni wakati wake tu ulikuwa umefika, hata wewe na yule zamu yako ikifika utakuwa tu juu.

Nachowashauri wenzangu haina haja ya kulazimisha umaarufu jitahidi ufanye kazi kwa bidii na uwe mbunifu kwa kile ukifanyacho kazi yako itakupandisha juu na kamwe hutoshuka ila ukilazimisha umaarufu utasikika kwa muda tu na kisha kupotea kabisa.

Kwa kina dada wale wanaopiga picture za utupu ili wapate umaarufu mwisho wa siku utaambulia umaarufu wa kudharauliwa na unakwisha kwa muda mfupi.

Umaarufu wa Dkt. Shika umekuja baada ya kujitokeza katika mnada wa  kuuza nyumba za Lugumi ambapo Dk. Shika aliahidi kununua nyumba hizo kwa thamani ya Sh bilioni 2.3 lakini alishindwa kulipia asilimia 25 ya fedha hizo ambazo ni shilingi milioni 800.

Post a Comment

Kwa maoni na ushauri weka comment yako hapo chini:

Previous Post Next Post