Ratiba ya michuano ya kombe la Mapinduzi imetolewa ambapo mabingwa watetezi, Azam FC wataanza na Jamhuri katika mchezo utakaofanyika uwanja wa Amaan Januari 2 mwaka 2018, kuanzia saa 10:15 jioni.
Simba SC ambayo ilicheza fainali na Azam FC mashindano yaliyopita itafungua dimba na URA ya Uganda katika michuano hiyo Januari 2, mwaka 2018 uwanja wa Amaan, Zanzibar mchezo ambao utaanza saa 2:15 usiku.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara Yanga, wataanza na JKU ya Zanzibar Januari 1, uwanja wa Amaan, mchezo huo utaanza saa 2:15 usiku.
Ufunguzi rasmi wa Kombe la Mapinduzi 2018 utafanyika Desemba 30, mwaka huu kwa mechi mbili kuchezwa Uwanja wa Amaan, kwanza Zimamoto na Mlandege Saa 10:17 jioni na baadaye JKU na Shaba Saa 2:15 usiku.
Tags
Michezo