Nyumba ya mwanzilishi wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria itabadilishwa na kufanywa jumba la makumbusho , serikali imetangaza.
Mamlaka
ya jimbo la Borno, Kaskasini mashariki mwa Nigeria imesema kuwa ujenzi
wa jumba hilo la makumbusho litapiga jeki utalii na elimu kwa vizazi
vijavyo kuhusu mienendo ya kundi hilo na hatari zake.Wanasema kuibadilisha nyumba ya Mohammed Yusuf aliyeuawa kuwa jumba la makumbusho kutasaidia kuhifadhi mabaki yanayohusiana na mashambulizi ya kundi hilo.
Lakini hatua hiyo imedaiwa kuzua maswala nyeti , huku wakosoaji wakisema itafufua vidonda vya walioathiriwa.
Nyumba hiyo ya Yusuf mjini Maidugiri ndipo eneo ambalo mzozo huo ulianza.
Alipigwa risasi alipokuwa kizuizini 2009 hatua ambayo ililikasirisha wanachama wa kundi la Boko Haram ambao walizidisha ghasia.
Mashambulio ya Boko Haram yamesababisha vifo vya takriban maelfu ya watu huku mamilioni ya raia wakiwachwa bila makao.
Tags
Kimataifa