Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku alifaa kupewa marufuku kwa kumpiga teke mlinzi wa Brighton Gaetan Bong, mchanganuzi wa maswala ya soka wa BBC Ian Wright amesema.
Kisa hicho kilitokea wakati klabu hiyo ilipopata ushindi wa 1-0 siku ya Jumamosi, lakini hakuonekana na refa Neil Swarbrick.
Jopo la shirikisho la soka nchini humo liliamua kwamba hafai kuchukuliwa hatua yoyote.
''Iwapo wataangalia tena, kwa nini wasione kwamba kilichofanyika kilikuwa makosa anafaa kuadhibiwa? Ndio'', Wright aliambia BBC Radio 5 live.
''Mara nilipoona nidhani wataingalia mara ya pili. Unafikiria ni kwa nini ameepuka''?
Tags
Michezo