Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz ameachia wimbo mpya wenye simulizi ya kinachomshinda katika kuishi maisha ya mahusiano ambapo hakuacha kusimuliza juu ya tukio lililotokea mpaka kupata mtoto wake wa tatu ‘Prince Abdul’ kwa mrembo Hamisa Mobetto.
Diamond Platnumz kama ilivyo kawaida yake kuyazungumzia mapenzi kwa malalamiko hakuacha kuwahusisha mtayarishaji wa kazi hiyo Lizer na dada yake Esma jinsi walivyomshauri juaa ya patashika alizokutana nazo katika mapenzi ya wapenzi aliowapenda mpaka kufikia hatua ya kutia nanga nzito kwa mama wa watito wake Zarinah Hassan ‘Zari The BossLady’
Tags
Urembo